• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Malalamiko na Mrejesho |
    • Barua pepe za watumishi |
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Malengo
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha & Biashara
      • Afya
      • Kilimo,Ushirika na Umwagiliaji
      • Ujenzi & Zimamoto
      • Maendeleo Ya Jamii
      • Mazingira & Usafishaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • MIfugo & Uvuvi
      • Ardhi & Maliasili
      • Water
    • Vitengo
      • TEHAMA & Uhusiano
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Nyuki
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Water
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu.
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Ripoti Mbalimbali
      • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Video

Serengeti wanufaika na uwekezaji wa Singita Grumeti.

Imewekwa: February 17th, 2017

Mfuko wa Singita Grumeti umeendelea kuwa mstari wa mbele katika kuboresha hali ya elimu katika Wilaya za Serengeti na Bunda.Hii imedhihirika kwenye halfa ya kukabidhi madawati 500 kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk. Charles Mlingwa ili kupunguza uhaba wa madawati katika Wilaya hizo. Aidha Grumeti wamekabidhi nyumba ya kuishi mwalimu iliyojengwa katika Shule ya Msingi Makundusi.

“Tuko hapa kukabidhi madawati haya 500 yenye thamani ya Tshs. Milioni 112 kwa Wilaya za Serengeti na Bunda pamoja na nyumba hii yenye thamani ya Tshs. Milioni 86” alisema Richard Ndaskoi ambae ni Mkuu wa Huduma za Jamii toka Mfuko wa Singinta Grumeti.

Akipokea misaada hiyo, Dk. Mlingwa alisema “Nawashukuru Singita Grumeti kwa Msaada huu wa madawati pamoja na nyumba hakika mchango wenu katika Mkoa wa Mara unaoneka” Dk Mlingwa amewataka wawekezaji wengine katika Mkoa wa Mara kuchangia madawati katika Wilaya za Serengeti na Bunda kwani bado zina uhaba wa madawati. 

Aidha Dk. Mlingwa ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti kwa kuwa na mahusiano mazuri na wawekezaji waliopo katika Wilaya hiyo “Tukiwawekea mazingira mazuri ya kufanya shughuli zao hata wananchi pia watanufaika na uwepo wa wawekezaji hawa” alisema Dk. Mlingwa.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili wote kwa nyakati tofauti wameushukuru Mfuko wa Singita Grumeti kwa msaada huo wa madawati na kuuomba mfuko huo kuendelea kuchangia katika shughuli za maendeleo katika Wilaya za Serengeti na Bunda. “Wilaya hii ina wawekezaji wengi lakini wamekuwa nyuma katika kuchangia shughuli za maendeleo, nawapongeza kwa kuwa mstari wa mbele kusaidia jamii inayowazunguka pamoja na kuchangia katika maendeleo ya Wilaya ya Serengeti” alisema Nurdin Babu.

Aidha Bi. Bupilipili ameuomba Mfuko huo kuanzisha kampeni maalumu ya kuongeza kiwango cha ufaulu kwa watoto wa kike kwa shule za sekondari Wilayani Bunda.Singita Grumeti wamekuwa wawekezaji wenye tija kwa wananchi wa Wilaya za Serengeti na Bunda licha ya kuwa mstari wa mbele kuchangia katika shughuli za maendeleo, kampuni hiyo pia imekuwa ikitoa ajira kwa wakazi toka wilaya hizo mbili pamoja na kutoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi toka wilaya hizo.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI AWAMU YA PILI KWA WAENDESHA BVR NA WAANDISHI MSAIDIZI April 28, 2025
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU. March 07, 2025
  • TANGAZO LA KUTOA MAONI KUHUSU SHERIA NDOGO. February 24, 2025
  • TANGAZO KWA UMMA January 02, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • SIKU YA MALARIA WILAYANI SERENGETI

    April 25, 2025
  • KAMATI YA FEDHA UONGOZI NA MIPANGO WATEMBELEA ENEO LA UJENZI WA JENGO LA UTAWALA.

    April 16, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI SERENGETI LAPITISHA BILIONI 48.8 KAMA MPANGO WA BAJETI YA HALMASHAURI 2025/2026.

    March 04, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI WILAYANI SERENGETI LAPITISHA MPANGO WA BAJETI YA TARURA BILIONI 2.4

    March 03, 2025
  • Angalia zote

Video

AKINA MAMA SERENGETI WASEMA ASANTE MAMA SAMIA.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Maktaba ya Picha za Matukio mbali mbali
  • Matokeo ya Kidato cha nne mwaka 2017
  • Bofya hapa kupata fomu mbalimbali za Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • UCHAGUZI KIDATO CHA KWANZA 2022 SERENGETI DC
  • FOLLOW US INSTAGRAM
  • Matokeo ya upimaji wa kitaifa wa Kidato cha pili (FTNA) 2017
  • FOLLOW US TWITTER

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu ya Rais
  • Utumishi
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Sekretarieti ya Mkoa wa MARA
  • Tanzania National Parks TANAPA
  • Frankfurt Zoological Society (FZS)

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    31603 Stendi Kuu | Serengeti

    Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti

    Simu ya mezani: 0282985686

    Simu: 0782677763

    Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz

Other Contacts

   

Wageni waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti