Kamati ya Fedha,mipango na Uongozi ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti ambae pia ni Diwani wa Kata ya Busawe Mhe.Ayub M.Makuruma wametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Shule ya sekondari Morotonga .
Shule ya sekondari Morotonga inajengwa kwa fedha kutoka serikali Kuu kupitia mpango wa kuboresha Maendeleo ya shule za sekondari hapa Nchini SEQUIP.
Shule hiii inajengwa Kata ya morotonga ,Kijiji cha Romakendo,Kupitia mpango huu serikali ilitoa kiasi cha Tsh.470,000,0000/=Kwa ajiri ya ujenzi wa shule hiyo Ambapo fedha hiyo inatarajiwa kujenga Vyumba 08 vya madarasa,Maabara 03 za sayansi,chumba cha ICT , Jengo la utawala,Maktaba,Matundu 20 ya vyoo(10 wasichana na 10 wavulana ),Kujenga miundombinu ya kuvunia Maji lita elfu 10,Kununua Tank la Maji la lita 10 na kujenga miundombinu ya kunawia maji.
Mradi huu ulianza kutekelezwa mnao Machi 1,2022.kwa kupitia Mradi wa maendeleo Gereza Mugumu Tabora B ambapo atajenga mpaka hatua ya finishing.
Mhe.Makuruma amepongeza kasi iliyopo katika ujenzi huo na kusisitiza wananchi kujitokeza kushiriki katika ujenzi huo na kulinda mali zilizopo eneo la ujenzi,aidha ameishukuru serikali Kuu inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassani kwa kuendelea kuimbuka wilaya ya Serengeti kwa kuleta miradi mbalimbali.
Ujenzi huu unategemewa kukamilika Mnamo 27 Juni 2022.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti