• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Malalamiko na Mrejesho |
    • Barua pepe za watumishi |
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Malengo
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha & Biashara
      • Afya
      • Kilimo,Ushirika na Umwagiliaji
      • Ujenzi & Zimamoto
      • Maendeleo Ya Jamii
      • Mazingira & Usafishaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • MIfugo & Uvuvi
      • Ardhi & Maliasili
      • Water
    • Vitengo
      • TEHAMA & Uhusiano
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Nyuki
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Water
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu.
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Ripoti Mbalimbali
      • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Video

SIKU YA HEDHI SALAMA DUNIANI | GRUMETI FUND YATOA TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI 640 SERENGETI

Imewekwa: May 28th, 2023

IKU YA HEDHI SALAMA DUNIANI | GRUMETI FUND YATOA TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI 640 SERENGETI


Kampuni ya Grumeti Fund kupitia idara yake ya maendeleo ya jamii Leo mei 28,2023 imeadhimisha siku ya hedhi salama duniani kwa kutoa msaada wa taulo za kike zenye thamani ya zaidi ya million 8, zinazoweza kutumika kwa kipindi Cha mwaka mmoja na nusu (reusable pads) kwa zaidi ya wanafunzi wa kike 640 kutoka katika shule za sekondari Serengeti na Nyichoka zilizopo wilayani Serengeti mkoa wa Mara.

Akikabidhi msaada huo mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii ya kampuni ya Grumeti Fund, Frida Mollel amewasihi wasichana hao kuwa hedhi sio ugonjwa bali ni kitu cha asili kwa mwanamke na hakipaswi kuwa sababu ya kuzuia binti kufikia ndoto zake.

kwa upande wa mkufunzi kutoka chuo cha afya Kisare Mwl.Restuda Murutta amewasisitiza wanafunzi hao kuzingatia usafi wawapo katika kipindi cha hedhi ili kuepuka madhara yanayoweza kutokana na uchafu wakati wa hedhi na utupaji sahihi wa taulo za kike.

Aidha wanafunzi hao wameelimishwa juu ya kukabiliana na mimba za utotoni kwa kuchukua tahadhari kwa kuondokana na tamaa za kumiliki vitu pamoja na kutokuwa na makundi mabaya.


kwa upande wao wanafunzi wakieleza sababu zinazoweza kupelekea mimba za utotoni wamesema kukosa elimu ya kijinsia pamoja na kukosa hofu ya Mungu ni baadhi ya visababishi vikubwa vya mimba za utotoni.


Naye Mgeni rasmi katika mafunzo hayo Bi.Antusa Swai ameipongeza taasisi ya Grumeti Fund kwa kuadhimisha siku ya hedhi salama duniani kwa kutoa taulo za kike na mafunzo kwa wasichana hao.


"naipongeza sana taasisi ya Grumeti Fund kwa kutoa taulo hizi za kike,zitawasaidia kwa kipindi chote na msijiingize katika vitendo vibaya na kuwa tamaa kwa kukosa mahitaji muhimu cha msingi ni kuwa wavumilivu na kutumia rasilimali zilizopo ili ziwasaidie na hatimaye kuweza kutimia ndoto zenu" alisema Antussa


Grumeti Fund itaendelea kutoa elimu ya kijinsia kwa wavulana na wasichana wa shule za sekondari na kutoa taulo za kike kwa kila binti atakayeshiriki mafunzo hayo. Grumeti Fund inatarajia kuwafikia zaidi ya wavulana na wasichana 3,800 kwa mwaka huu 2023.

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAILI September 21, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA SERENGETI September 07, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI April 18, 2023
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI KIDATO CHA KWANZA 2023 December 13, 2022
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • DED SERENGETI AISHUKURU BENKI YA AZANI KWA MSAADA WA MAPIPA YA TAKA

    September 11, 2023
  • DC MASHINJI AONGOZA MAZOEZI YA UTAYARI KUELEKEA SIKU YA VIJANA DUNIANI

    August 05, 2023
  • DC MASHINJI AFANYA ZIARA KATA YA KIKAZI KATA YA KYAMBAHI

    July 22, 2023
  • MKUU WA WILAYA SERENGETI AONGOZA KIKAO CHA TATHMINI YA LISHE NDANI YA WILAYA

    July 20, 2023
  • Angalia zote

Video

DKT.MASHINJI ASITISH A SHUGHULIZA UCHIMBAJI KOKOTO KUFUATIA KIFO CHA MCHIMBAJI
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Maktaba ya Picha za Matukio mbali mbali
  • Matokeo ya Kidato cha nne mwaka 2017
  • Bofya hapa kupata fomu mbalimbali za Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • UCHAGUZI KIDATO CHA KWANZA 2022 SERENGETI DC
  • FOLLOW US INSTAGRAM
  • Matokeo ya upimaji wa kitaifa wa Kidato cha pili (FTNA) 2017
  • FOLLOW US TWITTER

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu ya Rais
  • Utumishi
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Sekretarieti ya Mkoa wa MARA
  • Tanzania National Parks TANAPA
  • Frankfurt Zoological Society (FZS)

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    31603 Stendi Kuu | Serengeti

    Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti

    Simu ya mezani: 0282985686

    Simu: 0782677763

    Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz

Other Contacts

   

Wageni waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti