• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Malalamiko na Mrejesho |
    • Barua pepe za watumishi |
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Malengo
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha & Biashara
      • Afya
      • Kilimo,Ushirika na Umwagiliaji
      • Ujenzi & Zimamoto
      • Maendeleo Ya Jamii
      • Mazingira & Usafishaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • MIfugo & Uvuvi
      • Ardhi & Maliasili
      • Water
    • Vitengo
      • TEHAMA & Uhusiano
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Nyuki
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Water
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu.
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Ripoti Mbalimbali
      • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Video

KAMPUNI YA GRUMETI FUND YAWAFUNDA WASICHANA BUNDA, SERENGETI DHIDI YA VITENDO VYA UKATILI NA KUJITAMBUA

Imewekwa: September 17th, 2022

Na. Mwihava, GF -SERENGETI


Kampuni ya Grumeti Fund kupitia idara yake ya maendeleo ya jamii imetoa mafunzo kwa wasichana 657 kupitia progam ya  girl's Empowerment  session tuko pamoja yaliyolenga  juu ya kujitambua ,kujisimamia na kujilinda dhidi ya vitendo vya ukatili  ikiwemo ukeketaji kwa mtoto wa kike. Sambamba na ugawaji wa taulo za kike  657 ambazo  hutukumika kwa mwaka mmoja ( reusable pads) kwa wasichana nao, kutoka shule za sekondari  Hunyari, Sazira na Paul Jones za Wilayani Bunda na shule za Sekondari Robanda na Mugumu  za Wilayani  Serengeti.

 

 Wasichana Kutoka Baadhi ya Shule Wilayani bunda na Serengeti wakifatilia mafunzo kwa Makini kutoka 

kwa wawezeshaji wakati wa Kongamano hilo wilayani Serengeti

Akifungua mafunzo hayo mgeni rasmi Bi.Rehema koka mkuu wa idara ya mifugo  wilayani  Serengeti amewasihi wasichana  hao kujisimamia na kutokukimbilia mila potofu lakini pia ameishukuru na  kuipongeza kampuni ya Grumeti Fund kwa kuweza kujitoa kuwapa elimu wasichana  katika Mkoa wa Mara ikiwemo Serengeti ,aidha amesisitiza wasichana hao kuhakikisha wanasoma kwa bidii ili kutimiza ndoto zao pamoja na kuwepo kwa vikwazo mbalimbali vinavyowazunguka.


                                                    Mgeni Rasmi katika kongamano hilo Bi Rehema koka akisema Jambo wakati wa mafunzo hayo.


‘’Najua katika kusoma mnapitia changamoto mbalimbali lakini changamoto mojawapo  ni ya Karo ambayo raisi wetu Samia Suluhu Hassani  ameitatua,pamoja na kutatuliwa kwa changamoto hiyo  zipo changamoto za mila potofu zinazomuathiri mtoto wa kike,Hedhi ambayo huwatesa baadhi ya wasichana na kuwapotezea muda kutokana na visumbufu vichache,lakini pia umbali baadhi ya watoto wa kike pamoja na changmaoto ya kukatishwa tamaa’’alisema Bi.Rehema


Nae,Meneja wa maendeleo  ya jamii kutoka kampuni ya Grumeti Fund  Bi.Frida mollel amewataka wasichana kujitambua na kujitegemea bila kusubiri watu wengine kuwafanyia maamuzi ya maisha yao haswa katika vitu visivyofaa vinavyoharibu maisha yao ya sasa na baadae.

                                                           Meneja wa Idara ya Maendeleo ya Jamii kutoka Kampuni ya Grumeti Fund Bi.Frida Mollel akisema Jambo wakati wa Kongamano hilo


 ‘’Sisi Grumeti Fund tumekuja hapa kuwapa nguvu na kuwambia kwamba mabinti mnahaki ya elimu,lakini mnahaki ya kusema hapana dhidi ya mila potofu zinazowagandamiza  ikiwemo ndoa za utotoni,ukeketaji,mimba za utotoni mnahaki ya kujisimamia na kuachana na makundi potofu’’alisistiza Bi.Frida


Mtaalamu wa afya kutoka hospitali  teule ya nyerere (NDDH  )Bi.Restuna mluta amewakumbusha wasichana waliohudhuria mafunzo hayo kuwa wanapoonza hedhi ni kiashiria kwamba wako tayari kubeba ujauzito na kuitwa mama,amewataka kuzingatia umri salama wa wao kupata mimba kwani kupata ujauzito katika umri mdogo kunaweza kupelekea madhara kwa mama na mtoto ataezaliwa, aidha amewataka wasichana kujikinga kwa mimba za utoto kwa kusema hapana ,lakini pia kuzingatia masomo  na hatimaye kutimiza ndoto zao.


                                                                        Muwezeshaji Katika kongamano hilo Bi.Sijali Nyambuche afisa dawati la Jinsia na Watoto wilayani Serengeti akitoa mafunzo.


Kwa upande wa Afisa dawati la jinsia  na watoto wilaya ya Serengeti Bi. Sijali Nyambuche amewafundisha wasichana aina mbalimbali za ukeketaji lakini pia amewakumbusha  kuwa mkoa wa Mara ni miongoni mwa mikoa inayotekeleza vitendo vya ukeketaji  hivyo amewataka wasichana kutokukubali vitendo hivyo kutokana na madhara makubwa yanayojitokeza kutokana na kukeketwa hivyo amewataka wasichana hao kufika katika maeneo salama ili kutofanyiwa vitendo hivyo.




Nao wasichana waliopata mafunzo hayo kupitia kongamano hilo wameishukuru kampuni ya Grumeti Fund kwa kuweza kuwapa elimu hiyo na kuiomba serikali na wadau wengine kuongeza Zaidi makongamano ya aina hiyo ili kuweza kuelimika Zaidi.


                                                                                     Mgeni Rasmi Bi.Rehema koka akigawa Mataulo ya kike kwa wasichana 657 waliofika kwenye kongamano hilo

Mafunzo hayo yamewakutanisha wasichana kutoka katika baadhi ya shule zilipo wilaya ya bunda na Serengeti,ambapo yalifadhiliwa na kampuni ya Grumenti Fund

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA SERENGETI. June 11, 2025
  • ORODHA YA MAJINA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI AWAMU YA PILI KWA WAENDESHA BVR NA WAANDISHI MSAIDIZI April 28, 2025
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU. March 07, 2025
  • TANGAZO LA KUTOA MAONI KUHUSU SHERIA NDOGO. February 24, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • WADAU WA ZAO LA TUMBAKU WATAKIWA KUZINGATIA MIONGOZO YA KILIMO CHA ZAO LA TUMBAKU ILI KUPATA TIJA YA ZAO HILO.

    June 17, 2025
  • WANANCHI WA KIJIJI CHA PARK NYIGOTI SERENGETI WANUFAIKA NA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KUTOKA GRUMETI FUND.

    June 13, 2025
  • GRUMETI FUND YAENDELEA KUGUSA MAISHA YA VIJANA WA KIKE NA KIUME WILAYANI SERENGETI.

    June 04, 2025
  • SIKU YA MALARIA WILAYANI SERENGETI

    April 25, 2025
  • Angalia zote

Video

AKINA MAMA SERENGETI WASEMA ASANTE MAMA SAMIA.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Maktaba ya Picha za Matukio mbali mbali
  • Matokeo ya Kidato cha nne mwaka 2017
  • Bofya hapa kupata fomu mbalimbali za Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • UCHAGUZI KIDATO CHA KWANZA 2022 SERENGETI DC
  • FOLLOW US INSTAGRAM
  • Matokeo ya upimaji wa kitaifa wa Kidato cha pili (FTNA) 2017
  • FOLLOW US TWITTER

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu ya Rais
  • Utumishi
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Sekretarieti ya Mkoa wa MARA
  • Tanzania National Parks TANAPA
  • Frankfurt Zoological Society (FZS)

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    31603 Stendi Kuu | Serengeti

    Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti

    Simu ya mezani: 0282985686

    Simu: 0782677763

    Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz

Other Contacts

   

Wageni waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti