• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Malalamiko na Mrejesho |
    • Barua pepe za watumishi |
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Malengo
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha & Biashara
      • Afya
      • Kilimo,Ushirika na Umwagiliaji
      • Ujenzi & Zimamoto
      • Maendeleo Ya Jamii
      • Mazingira & Usafishaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • MIfugo & Uvuvi
      • Ardhi & Maliasili
      • Water
    • Vitengo
      • TEHAMA & Uhusiano
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Nyuki
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Water
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu.
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Ripoti Mbalimbali
      • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Video

GRUMETI FUND YAGUSA MAISHA YA VIJANA ZAIDI YA 1000 MKOA WA MARA

Imewekwa: September 30th, 2024

SHIRIKA la Grumeti Fund  kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii imewaleta pamoja Wanafunzi wa kike 688 na wakiume 610 kutoka katika shule za Kunzugu, Sizaki na Paul Jones sekondari zilizopo Wilayani Bunda, kwa lengo la kutoa Elimu sambamba na kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili watoto wa kike na kiume pamoja na utatuzi wake ili kujenga jamii yenye usawa miongoni mwa vijana wa jinsia zote.

Katika kongamano lililofanyika kwa siku mbili katika shule ya Sekondari Kunzugu yakihusisha wanafunzi wa kike na kiume, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii kutoka Grumeti Fund Bi. Frida Mollel amesema  lengo la Grumeti Fund kufanya kongamano hilo ni kuwaelimisha  vijana wa kike na kiume kutambua thamani yao sambamba na kuwajengea uwezo wa kujiamini na kufikia ndoto zao huku akiwataka kumtanguliza Mungu katika kila jambo kwani ndio msingi wa mafanikio.

"Vijana wengi sasa wametumbukia katika tabia hatarishi ambazo kupitia tabia hizo ni ngumu kufikia ndoto zenu, ili muweze kufikia ndoto zenu na kuwa vijana wakutegemewa katika familia na taifa Kwa ujumla, mambo matatu muhimu ambayo ninyi kama vijana mnatakiwa kuyaweka mbele kwanza ni kumcha Mungu kwasababu ndio chanzo cha maarifa , pili, kujitambua na kujiamini, na kufanya bidii katika masomo.  Grumeti Fund, tumekuja kuwatia moyo kuwa unaweza kuwa mtu yeyote endapo utamtanguliza Mungu, ukitambua thamani yako na ukijiamini na kufanya bidii asitokee mtu atakayekwambia kuwa huwezi, nawataka mfahamu kwamba mnaweza"


Aidha, Bi. Frida amewataka vijana hao kutotumbukia katika matumizi mabaya ya utandawazi na kuwataka vijana hao kuitumia mitandao ya kijamii katika namna itakayowaongezea ujuzi katika kuzitimiza ndoto zao.

Katika kongamano hilo shirika la Grumeti Fund imetoa Mipira na jezi za mpira Kwa shule zote tatu zilizoshiriki kwa wanafunzi wa kiume na  msaada wa taulo za kike  zinazoweza kutumika  kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu (reusable pads) kwa wanafunzi wa kike 688 zenye thamani ya Shilingi 9,632,000/- katika shule za sekondari Kunzugu, Paul Jones na Sizaki.

Naye mgeni rasmi  katika kongamano la wasichana Bi. Pelesia Manyama ambaye ni Katibu wa chama cha Walimu, amewataka wasichana kuwekeza katika kumcha Mungu kwani Kwa Mungu ndipo msaada wa matatizo yote unapatikana.

"Niwaambie kuwa ukimcha Mungu utaepuka mambo mengi mabaya, hata sisi tulivyo hivi ni kwasababu tuliwekeza katika kumcha Mungu na bado tunamtegemea yeye hadi sasa, kwani mwanafunzi bila kumtegemea Mungu hautafika popote, dunia na tamaa zake zitakumeza. Ili kufanikiwa katika masomo yako jitahidi sana kuwa na hofu ya Mungu pamoja na kuwekeza katika kumcha Mungu" Jiepusheni na marafiki wabaya na mambo yasiyo na tija, Alisema Bi. Pelesia Manyama.


Kwa upande wake  mkufunzi kutoka  chuo cha Afya Kisare Mwl. Restuda Murutta akitoa Elimu ya uzazi kwa wanafunzi wa kike amewaasa kuzingatia usafi wawapo katika siku za hedhi na  kuwataka kuzitumia taulo za kike zilizotolewa na Grumeti Fund kwa usahihi sambamba na kuepuka vishawishi vitakavyo waingiza katika kufanya mapenzi katika umri mdogo na mwisho kupelekea ndoa za utotoni.

“Usafi wakati wa hedhi ni muhimu sana kwani utaepuka magonjwa mbalimbali, lakini pia inasikitisha binti anaumri chini ya miaka 18 ameshaanza kujiingiza kwenye mahusiano ya ngono kitu ambacho sio salama, kabla ya kuingia kwenye mambo hayo kwanza jiulize je ni umri sahihi wa kuingia kwenye mambo hayo ukishapata jibu acha" alisema Bi. Restuda


Naye aliyekuwa Mgeni rasmi katika kongamano la wanafunzi wa kiume  anayehudumia idara ya vijana katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Emmanuel Samuel Sitta amewaasa vijana wa kiume kujitambua kuwa wao ni wanaume na wameumbwa na Mwenyezi Mungu kama wanaume Kwa makusudi.

"Siku hizi imezuka tabia ya wanaume kutamani kufanya mambo ya jinsia ya kike, niwaambie kuwa wewe umeumbwa na Mungu kama mwanaume hivyo unatakiwa kufanya yale yaliyowekwa na Mungu ili yafanywe na wanaume na si vinginevyo " alisema Mchungaji Sitta.


Nao miongoni mwa wanafunzi wa kike na kiume waliopata mafunzo wameishukuru kampuni ya Grumeti Fund kwa namna wanavyowajali na kuwathamini vijana wa kike na kiume katika kujenga jamii bora yenye usawa na kuahidi kuyaweka katika vitendo mafunzo hayo na kusambaza elimu kwa wengine.

Kwa takribani miaka saba kampuni ya Grumeti Fund imekuwa ikitoa elimu ya kijinsia kwa wanafunzi wa kike na kiume katika shule za sekondari mbalimbali Wilayani Serengeti na Bunda ambapo tangu mwaka 2017 hadi awamu hii ya tatu  ya kongamano hili kwa Mwaka 2024  imefanikiwa kutoa elimu ya kijinsia kwa wasichana 12,397 na kutoa taulo 12,397  kwa kila binti anayeshiriki mafunzo hayo, huku ikifanikiwa kutoa mafunzo kwa wavulana zaidi ya 6,274 tangu mwaka 2021 hadi awamu hii  ya tatu ya kongamano la Mwaka 2024 na kutoa zawadi za jezi na mipira  kwa kila shule iliyoshiriki kwenye kongamano.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA SERENGETI July 01, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA SERENGETI. June 11, 2025
  • ORODHA YA MAJINA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI AWAMU YA PILI KWA WAENDESHA BVR NA WAANDISHI MSAIDIZI April 28, 2025
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU. March 07, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • BARAZA LA MAMLAKA YA MJI MDOGO SERENGETI LAZINDULIWA LEO.

    July 10, 2025
  • TSC SERENGETI YAENDESHA MAFUNZO ELEKEZI KWA WALIMU WAPYA 89.

    July 09, 2025
  • DAS MASIKO AKABIDHIWA OFISI.

    July 04, 2025
  • DC ANGELINA AKABIDHIWA OFISI

    July 04, 2025
  • Angalia zote

Video

AKINA MAMA SERENGETI WASEMA ASANTE MAMA SAMIA.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Maktaba ya Picha za Matukio mbali mbali
  • Matokeo ya Kidato cha nne mwaka 2017
  • Bofya hapa kupata fomu mbalimbali za Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • UCHAGUZI KIDATO CHA KWANZA 2022 SERENGETI DC
  • FOLLOW US INSTAGRAM
  • Matokeo ya upimaji wa kitaifa wa Kidato cha pili (FTNA) 2017
  • FOLLOW US TWITTER

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu ya Rais
  • Utumishi
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Sekretarieti ya Mkoa wa MARA
  • Tanzania National Parks TANAPA
  • Frankfurt Zoological Society (FZS)

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    31603 Stendi Kuu | Serengeti

    Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti

    Simu ya mezani: 0282985686

    Simu: 0782677763

    Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz

Other Contacts

   

Wageni waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti