• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Malalamiko na Mrejesho |
    • Barua pepe za watumishi |
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Malengo
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha & Biashara
      • Afya
      • Kilimo,Ushirika na Umwagiliaji
      • Ujenzi & Zimamoto
      • Maendeleo Ya Jamii
      • Mazingira & Usafishaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • MIfugo & Uvuvi
      • Ardhi & Maliasili
      • Water
    • Vitengo
      • TEHAMA & Uhusiano
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Nyuki
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Water
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu.
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Ripoti Mbalimbali
      • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Video

Mshauri wa Tasaf Ndugu Sokoro Mnubi amekamirisha zoezi la uwasilishaji wa Fedha za Kaya Masikini Tarafa ya Ngoreme pamoja na Ikorongo 19/02/2021

Imewekwa: February 19th, 2021

Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti leo 19/02/2021 imekamilisha zoezi la uwasilishaji  fedha kwa walengwa wa Kaya Masikini Tarafa ya Ngoreme kwenye Vijiji vya Nyamihuru,Nyamakobiti, Messaga, Nyagasense, Remung’orori na Msati.

Zoezi limefanyika vizuri bila uwepo wa malalamiko yoyote kwani wanufaika wote katika vijiji ambavyo vimetembelewa na  wawezeshaji akiwemo  Mshauri wa Tasaf Ndugu Sokoro Mnubi wamethibitisha kwamba zoezi limeenda vizuri bila malalamiko ya aina yoyote.

Katika Kijiji cha Nyamihuru  Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho Bi Happy Fanuel Mwita alithibitisha kuwa wamepokea Fedha Jumla ya Tsh 3,030,000/=  kwa ajili ya kuzigawa kwa walengwa hao ambao  jumla ya Idadi yao ni (49) ambapo alifanya mazungumzo na Afisa Habari wa Halmashauri ya Wilaya Serengeti na kumthibitishia kuwa fedha zinatumika vizuri hasa kwa kundi la Wanawake ambao wamekuwa wakizitumia kwa shughuli mbali mbali kama Ufugaji,Kilimo pamoja na Biashara lakini pia Mwenyekiti wa Kijiji hicho Ndugu David Chacha Mgendi.


                                  Happy Fanuel Afisa Mtendaji aliesimamia zoezi akiwa na Muwezeshaji Bwana Nyambita 

Baada ya maelezo hayo kutoka kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Nyamehuru na Mwenyekiti wa Kijiji hicho  ndipo Mshauri wa Tasaf  Ndugu Sokoro Mnubi alipata nafasi ya kuzungumza na wanufaika hao na kuwashauri juu ya matumizi mazuri ya fedha hizo na hasa katika kuzitumia fedha hizo pia kujiunga na Mfuko wa Afya wa CHF iliyoboreshwa ambayo inatolewa kwa Tsh 30,000/=.

                                                                    Davidi Chacha Mgendi Mwenyekiti Kijiji cha Nyamihuru

Ziara hio iliendelea mpaka katika Kijiji cha Nyagasense ambapo Mshauri wa Tasaf Ndugu Sokoro Mnubi alipokelewa na Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho Ndugu Mahitari Hunda pamoja na Mwenyekiti wa Kijiji hicho Ndugu Matiko Daniel Ngerecha ambao pia walithibitisha kwamba zoezi linaenda vizuri na ndio walikuwa wanakamilisha zoezi Majira ya Saa 7:38 Mchana ambapo pia alipata nafasi ya kuelezea changamoto za Mradi huo kwani walengwa ambao wanatokana na kundi la Wanaume wengi wao huzitumia vibaya Fedha hizo kwa kunywa pombe na tayari Serikali ya Kijiji imeshawaita na kuwaonya ili waweze kuacha tabia hizo lakini pia akachukua nafasi hio kuwapongeza kundi la akina Mama kwa matumizi mazuri ya fedha hizo ambazo zimewasaidia kujenga nyumba na kuanzisha biashara ndogondogo ambazo kwa sasa zinasaidia kuendesha familia zao.

Katika Kijiji cha Msati Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Msati Ndugu Mafuru Sagati amethibitisha kuwa wamepokea Fedha kiasi cha Tsh 3,048,000/= ambazo zimewasilishwa vizuri bila kuwepo kwa malalamiko yoyote ambapo Mwenyekiti wa Kijiji hicho Ndugu Mwita Daudi Mgendi amethibitisha kuwa fedha hizo zinatumiwa vizuri na walengwa hasa kwenye shughuli za Maendeleo.

                                                                                      Mafuru Sagati Afisa Mtendaji Kijiji cha Msati


Kijiji cha Remung’orori  kimepokea fedha kiasi cha Tsh 2,412,000/= Afisa Mtendaji wa Kata Ndugu Geofrey Innocent Mzee  ambaye ndie amesimamia zoezi hilo amethibitisha kuwa fedha hizo kwa Kjiji cha Remung’orori zinatumika vizuri na hakuna shida yoyote na kwamba wanufaika 48 kwa sasa ndio wanapokea fedha hizo.

                                                            Geofrey Innocent Mzee Afisa Mtendaji Kata Magange aliesimamia zoezi


Imetolewa 

Afisa Habari- Mahusiano

Emmanuel Isyaga Mwita

Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti.

Matangazo

  • FOMU ZA MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA JANUARI 2021 December 15, 2020
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA JANUARI 2021 December 21, 2020
  • ORODHA YA WANAFUNZI NA SHULE ZA SEKONDARI WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA 2021 SERENGETI. December 23, 2020
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA CHAGUO LA PILI SHULE ZOTE January 11, 2021
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Mhandisi Juma Hamsini atangaza Msiba wa Mtumishi Idara ya Afya Tabibu Mkuu Loti Misinzo

    March 07, 2021
  • Mwenyekti wa Chama cha Mapinduzi Mhe Jacob Bega na Mwenyekti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Ayub Mwita Makuruma waendelea na ziara Kata ya Nyamoko na Kebanchabancha

    March 01, 2021
  • Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mheshimiwa Jacob Bega na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Mheshimiwa Ayub Mwita Makuruma wafanya ziara ya kutembelea Kata kuhamasisha Maendeleo

    February 24, 2021
  • Wananchi Kata ya Kebancaha wajenga Sekondari Halamshauri ya Wilaya yapeleka Mbati 240,Mifuko ya Saruji 150 na Mbao 360 kuongeza nguvu

    February 20, 2021
  • Angalia zote

Video

Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Serengeti
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Maktaba ya Picha za Matukio mbali mbali
  • Matokeo ya Kidato cha nne mwaka 2017
  • Bofya hapa kupata fomu mbalimbali za Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Matokeo ya upimaji wa kitaifa wa Kidato cha pili (FTNA) 2017

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu ya Rais
  • Utumishi
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Sekretarieti ya Mkoa wa MARA
  • Tanzania National Parks TANAPA
  • GIZ

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    31603 Stendi Kuu | Serengeti

    Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti

    Simu ya mezani: 0282985686

    Simu: 0782677763

    Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz

Other Contacts

   

Wageni waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti