• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Malalamiko na Mrejesho |
    • Barua pepe za watumishi |
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Malengo
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha & Biashara
      • Afya
      • Kilimo,Ushirika na Umwagiliaji
      • Ujenzi & Zimamoto
      • Maendeleo Ya Jamii
      • Mazingira & Usafishaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • MIfugo & Uvuvi
      • Ardhi & Maliasili
      • Water
    • Vitengo
      • TEHAMA & Uhusiano
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Nyuki
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Water
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu.
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Ripoti Mbalimbali
      • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Video

MILIONI 120 KUKOPESHWA KWA VIKUNDI HAMSINI NA TANO

Imewekwa: December 10th, 2019

“Nyinyi vikundi hamsini na tano (55) mmeaminika, mmechujwa na mmeonekana kwamba mmekidhi vigezo ambavyo vimewekwa kwa ajili ya kupewa mikopo”

Hayo ni maneno ya Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Mh. Nurdini Babu aliyekuwa mgeni rasmi wakati akifungua mafunzo kwa vikundi kuhusu namna ya kutumia kwa tija mikopo inayotolewa na serikali. Mafunzo yaliyofanyika leo tarehe 10/12/2019 katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri

Babu amesema kuwa mikopo hiyo inayotolewa na serikali kupitia makusanyo ya halmashauri ipo na inawahusu wananchi wote ambao wapo tayari kujiunga kwenye vikundi vya uzalishaji mali pamoja na kukidhi masharti na taratibu za kuweza kupatiwa mkopo.

“Fedha hizi ni kwa mujibu wa sheria, lazima kwenye mapato ya ndani ya Halmashauri tutenge asilimia kumi (10%) kwa ajili ya vikundi mbalimbali, asilimia nne (4%) Wanawake, asilimia nne (4%) Vijana na asilimia mbili (2%) watu wenye Ulemavu”. Amesisitiza babu.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Mh. Juma Porini amesema kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Raisi Dr. John Magufuli imeondoa riba kwa vikundi vyote vinapochukua mkopo kutoka Halmashauri lengo likiwa ni kuwaondolea umasikini watanzania hasa wanawake, vijana na walemavu.

“Hatuchaji riba ya aina yoyote kwa hiyo hakuna hata mmoja asiyependa mkopo ambao hauna riba, kama ambavyo nyie mlipata hii fursa, iwe ni lazima na nyie kurudisha kwa wakati ili na wengine pia wapate hiyo fursa ya kukopa bila riba” Amesema Porini.

Image may contain: 5 people, including Juma Porini, people sitting

Mh. Porini akizungumza jambo

Awali akizungungumza wakati wa kutoa taarifa fupi kwa mgeni rasmi; Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya Bw. Wambura Sunday amesema kuwa mikopo hiyo hutolewa kwa vikundi ambavyo tayari vimeshatembelewa na kufanyiwa tathimini na kuona kuwa wanastahili kupewa mikopo, wanaelekezwa namna ya kufanya marejesho, elimu ya ujasiriamali pamoja na elimu ya kuweka na kukopa, na kwa sasa watatoa jumla ya Tshs. Milioni mia moja na ishirini (120,000,000) kwa vikundi vyote hamsini na tano.

Pia Wambura amewapongeza watumishi wa idara ya maendeleo ya jamii, watendaji kata na viongozi wa serikali za mitaa kwa kushirikiana kwa pamoja kusimamia vikundi na kuhakikisha vile vinavyokidhi vigezo ndivyo vinavyopatiwa mkopo ili viweze kuzalisha na kurejesha mikopo hiyo.

Kwa upande wao wanavikundi waliopata mafunzo hayo kutoka Halmashauri ya wilaya ya Serengeti wameishukuru serikali kwa kuwapatia mafunzo hayo na hatimaye kuwapa mkopo usiokuwa na riba na kusema kuwa wamefurahishwa na hatua hiyo na kwamba shughuli za vikundi hivyo zitafanyika kwa ufanisi baada ya mkopo huo usiokuwa na riba.

Aidha wameahidi kuirejesha mikopo hiyo mapema ili kuwapa nafasi wananchi wengine waweze kukopa.

Image may contain: one or more people, people sitting, crowd and indoor


Image may contain: 2 people, people sitting, table and indoor

Wanavikundi mbalimbali wakisikiliza maelekezo kwa makini

Katika robo hii ya kwanza ya mwaka wa fedha 2019/2020 jumla ya Vikundi hamsini na tano (55) vinatarajiwa kupewa jumla ya Tshs. Milioni mia moja na ishirini (120,000,000) kutoka katika asilimia 10 ya makusanyo ya mapato ya ndani ya Halmashauri ikiwa vikundi thelatini vya wanawake (Tshs. Milioni sitini), vikundi kumi na tisa vya vijana (Tshs. Milioni hamsini) na vikundi sita vya watu wenye ulemavu (Tshs. Milioni kumi) vitanufaika na mkopo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti ili kuwaongezea wananchi husika uwezo wa kujiongezea kipato na kurejesha fedha hizo bila riba ili ziweze kuwasaidia wengine kuinuka kiuchumi.

Matangazo

  • FOMU ZA MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA JANUARI 2021 December 15, 2020
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA JANUARI 2021 December 21, 2020
  • ORODHA YA WANAFUNZI NA SHULE ZA SEKONDARI WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA 2021 SERENGETI. December 23, 2020
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA CHAGUO LA PILI SHULE ZOTE January 11, 2021
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZINDUZI WA BARAZA LA MADIWANI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SERENGETI DESEMBA, 11th 2020

    December 11, 2020
  • WILAYA YA SERENGETI YAPATA MWENYEKITI MPYA WA HALMSAHURI

    December 11, 2020
  • RUWASA YAFANYA MKUTANO WA PILI NA WADAU WA MAJI NA USAFI WA MZINGIRA

    August 24, 2020
  • WASIMAMIZI WASAIDIZI WA UCHAGUZI NGAZI YA KATA WATAKIWA KUZINGATIA KATIBA NA SHERIA ZA UCHAGUZI KATIKA KUSIMAMIA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2020

    August 08, 2020
  • Angalia zote

Video

Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Serengeti
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Maktaba ya Picha za Matukio mbali mbali
  • Matokeo ya Kidato cha nne mwaka 2017
  • Bofya hapa kupata fomu mbalimbali za Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Matokeo ya upimaji wa kitaifa wa Kidato cha pili (FTNA) 2017

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu ya Rais
  • Utumishi
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Sekretarieti ya Mkoa wa MARA
  • Tanzania National Parks TANAPA
  • GIZ

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    31603 Stendi Kuu | Serengeti

    Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti

    Simu ya mezani: 0282985686

    Simu: 0782677763

    Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz

Other Contacts

   

Wageni waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti