• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Malalamiko na Mrejesho |
    • Barua pepe za watumishi |
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Malengo
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha & Biashara
      • Afya
      • Kilimo,Ushirika na Umwagiliaji
      • Ujenzi & Zimamoto
      • Maendeleo Ya Jamii
      • Mazingira & Usafishaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • MIfugo & Uvuvi
      • Ardhi & Maliasili
      • Water
    • Vitengo
      • TEHAMA & Uhusiano
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Nyuki
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Water
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu.
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Ripoti Mbalimbali
      • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Video

JIMBO LA SERENGETI LAENDESHA MAFUNZO KWA MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI NGAZI YA KATA

Imewekwa: July 24th, 2019

Leo tarehe 24/07/2019 ofisi ya Afisa Mwandikishaji Jimbo la Serengeti imeendesha mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa Maafisa Waandikishaji Wasaidizi wa Kata zilizopo katika Jimbo la Serengeti.

Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ambapo wawezeshaji walikuwa ni Maafisa Waandikishaji Wasaidizi wa Jimbo, Afisa Uchaguzi wa Wilaya na Afisa TEHAMA wa Wilaya

Bw. Nyambita Zakayo (Afisa TEHAMA wa Wilaya) akitoa mafunzo kwa washiriki wa semina (hawapo Pichani

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo Mgeni rasmi ambaye ni Afisa Mwandikisahaji Msaidizi Jimbo, kwa niaba ya Afisa Mwandikishaji Ndg. Victor Rutonesha alisema “Mafunzo haya yatahusisha ujazaji wa fomu zote zitakazotumika katika zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na mafunzo kwa vitendo yatakayohusu namna ya kutumia mashine za kusajilia (BVR Kits)”

Pia Ndg. Rutonesha ameongezea kwa kusema “mafunzo ya jinsi ya kutumia mfumo wa Uandikishaji yanalenga kuwawezesha Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Kata kupata uelewa wa jinsi ya kutumia kwa ufasaha BVR Kit kwa ajili ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na wao waweze kutoa mafunzo hayo kwa BVR Kit – Opereators na Waandishi Wasaidizi ambao ndio watahusika na uandikishaji wa Wapiga Kura vituoni”

Aidha Ndg. Rutonesha amewataka Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Kata waliowahi kushiriki zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa Miaka iliyopita kutumia uzoefu walioupata kuwasaidia Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Kata ambao hawakuwahi kushiriki katika mazoezi yaliyokwishapita

“Ni matumaini yangu kuwa, kwa kutumia uzoefu mlionao, mtafanya kazi zenu kwa ufanisi mkubwa, kwa bidi na moyo wa kujituma ili kufanikisha zoezi hili. Vile vile mtatumia uzoefu wenu mlionao kuwasaidia wenzenu ambao hawakuwahi kushiriki katika zoezi lililopita kutekeleza majukumu yao kikamilifu” alisema Ndg. Rutonesha

Pia Ndg Rutonesha amewakumbusha Maafisa hao kuwa Mawakala wa vyama vya siasa wanaruhusiwa kuwepo katika vituo vya Kuandikishia Wapiga Kura kwa kuwa jambo hilo ni muhimu na linasaidia kuleta uwazi katika zoezi zima la Uandikishaji. Lakini hawatakiwi kuwaingilia watendaji wanapotekeleza wajibu wao.

Baadhi ya washiriki wa semina wakimsikiliza Mwezeshaji (hayupo pichani)

Na mwisho amewataka Maafisa hao kuwa na ushirikiano na wadau mbali mbali ili kuhakikisha zoezi hili linafanyika kwa ufanisi mkubwa.

“Ni muhimu uwepo ushirikiano mkubwa kati ya watendaji wote wa zoezi hili, vyama vya siasa na wadau wengine wote. Ninawasihi muwe na ushirikiano mzuri na wa karibu na waandikishaji ngazi ya Jimbo wakati wote mtakapokuwa mnahitaji ufafanuzi au maelekezo katika kazi yenu” alisema Ndg. Rutonesha

Washiriki wa semina wakifuatilia mada

Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wamesema kuwa mafunzo haya yatawasaidia katika zoezi zima la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na wanaahidi watafanya kazi hii kwa utiifu na weledi wa hali ya juu ili kuhakikisha zoezi hili linafanyika kwa ufanisi mkubwa

Naye Afisa Mwandikishaji Jimbo Mhandisi Juma Hamsini aliwasisitiza Maafisa Waandikishaji Wasaidizi wa ngazi ya Kata kufanya kazi kwa Umakini, ufanisi na kuzingatia viapo walivyopokea katika utendaji wao.

Matangazo

  • TANGAZO KWA WANANCHI WOTE WALIOOMBA KUJENGA VIBANDA ENEO LA STENDI YA MABASI December 06, 2019
  • TANGAZO KWA WAZABUNI WOTE November 12, 2019
  • TANGAZO LA UUZAJI WA MICHE YA MITI April 10, 2019
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MH. RYOBA ALIA NA MABOMA

    August 16, 2019
  • WANANCHI WATAKIWA KUWA NA VIBALI VYA UJENZI

    August 10, 2019
  • JIMBO LA SERENGETI LAENDESHA MAFUNZO KWA MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI NGAZI YA KATA

    July 24, 2019
  • SERENGETI YAENDESHA SEMINA YA UHAKIKI WA TAARIFA ZA USULUHISHI WA KIBENKI (BANK RECONALIATION) KWA WAHASIBU

    July 04, 2019
  • Angalia zote

Video

Mkuu wa Wilaya ya Serengeti akiongelea kuhusu ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Serengeti.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Maktaba ya Picha za Matukio mbali mbali
  • Matokeo ya Kidato cha nne mwaka 2017
  • Bofya hapa kupata fomu mbalimbali za Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Matokeo ya upimaji wa kitaifa wa Kidato cha pili (FTNA) 2017

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu ya Rais
  • Utumishi
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Sekretarieti ya Mkoa wa MARA
  • Tanzania National Parks TANAPA
  • GIZ

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    31603 Stendi Kuu | Serengeti

    Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti

    Simu ya mezani: 0282985686

    Simu: 0782677763

    Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz

Other Contacts

   

Wageni waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti